Monday, 8 February 2016

MADIBIRA YANGU NA SERIKALI YETU

                                MADIBIRA TUNA KAA WATU 

                       Ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wa Madibira wakitazamwa kama wanyama wasio na uelewa wowote juu ya dunia hii.Watu mbalimbali wenye nafasi serikalini na wanasiasa wana ifanya sehemu hii kama sehemu isiyo na wanadamu au kama wapo hawana uelewa wowote. 

                                                   KILIMO

Image result for mpunga

Mwaka 1997 mradi wa kilimo cha umwagiliaji ulianzishwa Madibira na serikali ukiwa na eneo la hekta 6000 sawa na ekari 15000 ambazo zilizungushiwa tuta, shamba hili kubwa la umwagiliaji lipo chini ya wananchi wa kawaida. Shamba hili ni sawa na eneo lililoachwa linalo limwa na wananchi ambao wapo nje ya huo mradi. 

 

Image result for mpunga

Madibira nai moja ya wazalishaji wakubwa wa mpunga kwa Afrika Mashariki na kati, licha ya jitihada hizo serikali bado ipo mbali na watu hao.

                                               KIAFYA

             Toka miaka ya 70 ilijengwa zahanati ambayo baadae ikawa kituo cha Afya mpaka sasa, idadi ya watu kipindi kituo hiki kinajengwa haikuwa kama ilivyo sasa. inakadiliwa kuwa kulikuwa na watu 8000 tu kipindi kituo hicho kikijengwa, kwasasa kuna watu zaidi ya 32000 sawa na ongezeko la asilimia 300. mwanzoni mwa miaka ya 2000 ulifanyika ukarabati wa majengo mawili yaliyo kuwepo na liliongezwa jengo moja lenye vyumba viwili tu ambalo kwasasa linatumika kama wodi ya wanaume na wanawake.Kwamuda sasa wanasiasa (wabunge na madiwani) kila atakaye kuwa anatafuta nafasi ya kisiasa lazima atagusia kuboresha mazingira ya hospitali hii na wakishinda wanapotea. Kutokana na ongezeko hili la wana wakazi kumekuwa na shida sana,serikali imekuwa ikileta dawa kutokana na rekodi za nyuma ,hii inapelekea dawa kuisha mapema toka siku ya kuletwa kwake. Majengo machache na vitanda kwaajili ya kulazwa wagonjwa ni vichache, alipo kuja mheshimiwa rais aliahidi kutatua kero zote za wana mbarali na madibira kwa ujumla lakini chenga tupu.
                                                        ELIMU 

               Madibira ina shule za msingi zipatazo nane yaani; 

                                             Image result for SHULE YA MSINGI

                                           shule ya msingi Iheha

                                                
                         Image result for SHULE YA MSINGI MAHANGO MADIBIRA

                                        shule ya msingi mahango, 

                              Image result for SHULE YA MSINGI MADIBIRA

                           shule ya msingi chalisuka

                                     
                   Image result for JENGO LA SHULE    

                      shule ya msingi madibira,

             
                          Image result for WANAFUNZI

                                     shule ya msingi mkunywa 

                                
                      Image result for WANAFUNZI

                          shule ya msingi ikoga, 

          
                              Image result for WANAFUNZI SHULE YA MSINGI

                                                   shule ya msingi nyamakuyu 

                               Image result for WANAFUNZI SHULE YA MSINGI

                                          shule ya msingi nyakadete

Shule zote hizo zinatoa na kupeleka wanafunzi wao katika shule moja tu ya sekondari (shule ya sekondari madibira). 

              Image result for MADIBIRA SEKONDARI         Image result for MADIBIRA SEKONDARIImage result for MADIBIRA SEKONDARIImage result for MADIBIRA SEKONDARI

 Hata hiyo shule yenyewe walijenga wazazi na serilkali ikaongeza majengo miaka ya hivi karibuni wakati wa mpango wa kuanzisha kidato tano na sita shuleni hapo. Kwa shule za msingi hari sio nzuri sana kwani wanafunzi ni wengi na vyumba na samani ni chache kukizi mahitaji. walimu wengi wanakaa mitaani(hakuna nyumba za kutosha ). kwa upande wa sekondari ni yale yale.

                                   

   itaendelea............


                                                           

No comments:

Post a Comment